Kuanzisha klabu ya Agora Speakers ni rahisi sana; kuna mahitaji machache sana, na hakuna ada au taratibu zozote (hakuna ada ya katiba au manunuzi ya lazima ya aina yoyote).
Sharti la Kwanza la Mafanikio: Usijitahidi kuwa Mkamilifu
Jambo kuu ambalo linatofautisha klabu zilizofanikiwa na ambazo hazitofanikiwa ni kuwa klabu zinazofanikiwa hazitafuti ukamilifu. Utakapoanza kupanga mkutano wa kwanza, mfumo wako wa kufikiria utakuwa kama hivi "Hatuwezi kukutana Alhamisi ijayo kwasababu mvua inanyesha. Inayofuata ina ile mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, alafu tutakuwa na uchaguzi wa nchini". Tatizo na aina hii ya ufikiriaji ni kuwa haijalishi siku gani umechagua, he problem with this kind of reasoning is that no matter which day you pick, daima kutakuwa na kitu kinatokea kwenye siku hiyo.
Kamwe hakuwezi kuwa na muda sahihi wa kufanya uzinduzi. Klabu yenye mafanikio inafanya vitu SASA, inatenda makosa, na inajifunza haraka kutoka makosa yake. .
Hawasubirii muda muafaka kufanya uzinduzi. Hawasubiriii kutafuta ukumbi muafaka. Hawataki seti ya wanachama sahihi ili kupanga. Tafiti imeonyesha kuwa watu wakianza sasa, wakafeli harak, wanajifunza kutoka makosa yao, na kurudia wanakuwa na mafanikio zaidi na wanawasilisha matokeo ya hali ya juu kuliko watu ambao wanatathmini kila kitu kwa umakini, na ndio hapo wanaanza.
Daima kumbuka: Kama shughuli yenu inayofuata imepangwa zaidi ya wiki mbili mbele, sio tena kitendo - ni ndoto tu.
Mfululizo wa Uundaji wa Klabu
Mfululizo ufuatao unaonyesha hatua zilizopendekezwa ufuate ili kuunda klabu. Kwa kila hatua, muda umeonyeshwa.
Hata kama wewe ni mwanachama mzoefu wa klabu nyingine zinazofanana, ni muhimu ufuate kila hatua na usome kwa umakini kwani zina taarifa muhimu.